Monday, May 28, 2012

DKT.BILAL AZINDUA VITABU VIWILI VILIVYOTUNGWA NA YUSUPH MAKAMBA.



Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akionyesha Kitabu cha Binadam na kazi baada ya kukizindua kitabu hicho kilichotungwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Yusuph Makamba (kulia) wakati ya uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo, sambamba na hafla ya kumpongeza kwa kuitumikia nafasi yake ya Katibu Mkuu wa CCM hadi anastaafu. Kushoto ni Mke wa katibu huyo, Mama January Makamba.
Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Yusuph Makamba, akiwahutubia wageni waalikwa na wanachama wa CCM, waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa vitabu viwili vya Binadamu na Kazi na Ukweli kwa mujibu wa Biblia, na Kurani Tukufu, Suna za Mtume  na Sheria za nchi,alivyovitunga na kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Mwamvita Makamba wa kwanza wapili toka kushoto akiwa na baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya watu waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa vitabu viwili vya Binadamu na Kazi na Ukweli kwa mujibu wa Biblia, na Kurani Tukufu, Suna za Mtume  na Sheria za nchi uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo, sambamba na hafla ya kumpongeza Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Yusuph Makamba kwa kuitumikia nafasi yake ya Katibu Mkuu wa CCM hadi anastaafu.

No comments:

Post a Comment