Tuesday, May 22, 2012

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AMUAPISHA PROFESA MARK MWANDOSYA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

 Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum Profesa Mark Mwandosya akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.Na watatu kulia ni Karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gerson Mdemu.
Profesa Mwandosya akipokea miongozo ya kazi baada ya kula kiapo Ikulu leo asubuhi.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza na kumtakia mafanikio Profesa Mwandosya muda mfupi baada ya kumuapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsaidiaWaziri wa nchi katika ofisi ya Rais asiye na Wizara maalumu Profesa Mark Mwandosya kushuka katika ngazi za Ikulu baada ya kumuapisha leo asubuhi.
Waziri Profesa Mark Mwandosya akiwa katika mazungumzo na Rais Dkt. Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya kula kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.(picha na Freddy Maro).

No comments:

Post a Comment