Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bw.Joseph Kusaga akimkaribisha mgeni wake,Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mh Freeman Mbowe mapema leo mchana kwenye ofisi za kampuni hiyo,Mikocheni jijini Dae es Salaam
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe(kulia)akisalimiana na Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena Dina Marrios
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe(Kulia)akisalimiana na Mkuu wa idara ya kurekodi matangazo ya Radio, Dj Venture
Pichani kati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Clouuds Media Group,Bw.Joseph Kusaga akiwa na sehemu ya uongozi wa juu wa kampuni hiyo,wakifanya mazungumzo mafupi na Uongozi wa chama cha CHADEMA,ukiongozwa na Mwenyekiti wake Bw.Freeman Mbowe ambaye aliongozana na Mbunge wa jimbo la Ubungo,Mh John Mnyika pamoja na Ofisa Habari wa chama hicho,Bw.Tumaini Makene,na kufanya ziara fupi ya kuitembelea kampuni hiyo na kujionea mambo mbalimbali yanayofanywa na kampuni hiyo,mapema leo asubuhi,Mikocheni jijini Dar.
Mh.Freeman Mbowe akiwa ofisini kwa Bw.Joseph Kusaga wakizungumza machache mara baada ya kuwasili mapema leo mchana ndani ya mjengo wa kampuni hiyo,Mikocheni jijini Dar.
Mwenyekiti wa CHADEME,Mh.Freeman Mbowe akizungumza na Mbunge wa jimbo la Ubungo kwa tiketi ya chama hicho,Mh John Mnyika ambaye aliambatana na Ofisa habari wa chama hicho,Bw.Tumaini Makene,ndani ya ofisi ya Bw, Joseph Kusaga,Clouds Media Group,Mikocheni jijini Dar.
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni Bingwa ya Burudani nchini Primetime Promotion Juhayna Kusaga
No comments:
Post a Comment