Wednesday, May 30, 2012

RAIS KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA IVORY COAST JIJINI ARUSHA.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakiangalia shamba la kahawa wakati wakielekea  kwenye sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya AfDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakiwa katika mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya AfDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya kumbukumbu na mgeni wake Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast.
Tanzania inaunga mkono jitihada za Ivory Coast za kurudisha makao makuu ya Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB)  katika mji Mkuu wa Nchi hiyo Abidjan, ambapo ndipo yalikuwa makao makuu kabla ya vurugu za kisiasa nchini humo , zilizotokea mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa Octoba, 2010.
Kufuatia vurugu hizo, benki iliyahamishia makao makuu yake kwenda jijini Tunis, Tunisia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemueleza Rais Alassane Ouattara wakati wa mazungumzo yao leo asubuhi, katika hoteli ya Ngurdoto, mjini Arusha.
“Tunaunga mkono jitihada zenu za kurudisha Makao Makuu ya Benki ya Maendeleo ya Afrika, tunaelewa hali ambayo haikutegemewa na ya kusikitisha mliyopitia na ni vyema Benki ikarudi Abidjan” Rais Kikwete amemueleza Rais Outtara aliyewasili Arusha jana jioni 29 Mei, 2012.
Mbali na kuomba kuungwa mkono na nchi za Afrika na Benki ya Afrika, Rais Outtara, ambaye yuko nchini kwa mwaliko wa Rais Kikwete, amesema amekuja pia kutoa shukrani kwa Rais Kikwete kwa kusaidia katika kutatua mgogoro wao.
“Wa Ivoria wanakushukuru sana kwa msaada wako mkubwa wakati wa matatizo yetu, tunashukuru sana” Rais Ouattara amemuambia Rais Kikwete ambaye alikuwa mmoja wa wajumbe wa timu ya viongozi ya Umoja wa Afrika (AU) kushughulikia mgogoro wa Ivory Coast.
Timu hiyo ilikua chini ya Mauritania na wajumbe wengine walikua Afrika ya Kusini na Burkina Faso.
Akiwa nchini Rais Outtara pia anatarajiwa kuhutubia Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa AfDB ambao unafunguliwa kesho tarehe 31 Mei na Rais Kikwete, katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Arusha (AICC).


Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi Habari wa Rais, Msaidizi,
Arusha – Tanzania,
30 Mei, 2012 


No comments:

Post a Comment