Saturday, May 12, 2012

SIMBA KUPAMBANA NA AL-AHLY KESHO MJINI KHARTOUM SUDAN.

Washindi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Simba kesho itakuwa na kibarua cha kujihakikishia inasonga mbele katika mashindano ya kombe la shirikisho la CAF.
Simba SC waliondoka kuelekea  Khartoum Sudan tangu jummanne,  wakiwa na matokeo mazuri ya mchezo wa kwanza dhidi ya Al-Ahly  ulochezwa uwanja wa taifa Dar-es-salaam na Simba kuibuka na na ushindi wa 3-0.
“Tukiwa kama timu pekee ya Afrika Mashariki ilobaki katika mashindano tumefanya maandalizi yakutosha, kwakuwa tunajua Al-Ahly ni timu nzuri pia” alisema Kamwanga.
Wacheza 19 waliosafiri kwaajiri ya mtanange huo wa kesho mei 13,2012 ni Juma Kaseja, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Patrick Mafisango, Uhuru Seleman, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi and Emmanuel Okwi, Ali Mustapha, Obadia Mungusa, Victor Costa, Derrick Walulya, Jonas Gerald, Edward Christopher na Salum Machaku.
Viongozi ni Milovan Cirkovic (kocha mkuu), Amatre Richard (kocha msaidizi), Nico Nyagawa (co-ordinator), James Kisaka (goalkeeper’s coach), Cosmas Kapinga (doctor).

SOURCE ...MO BLOG 



No comments:

Post a Comment