Saturday, May 12, 2012

“SITAGOMBEA TENA URAIS NIKIFIKISHA MIAKA 75” RAIS MUSEVENI.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema hatogombea tena urais wa nchi yake atakapofikisha miaka 75, kama katiba ya Uganda inavyosema.
Akizungumza katika NTV Rais Museveni amesema utafiti wa kisayansi unadhibitisha kuwa mtu anaweza kuwa vizuri akifika miaka 75 ila hatoweza kuongoza kwa ufasaha na umakini.
 “nitakapofikisha miaka 75 sitokubaliana na kubadilishwa umri katika katiba ili mimi nipate tena nafasi ya kugombea urais” alisema Rais Museveni.
Kwasasa katiba inamruhusu Mh. Museveni kugombea tena sababu atakuwa chini ya miaka 75 uchaguzi wa 2016 japo akishinda atakuwa na miaka 77 kufikia 2021.


No comments:

Post a Comment