Wednesday, May 16, 2012

WAZIRI WA UCHUKUZI DK. HARRISON MWAKYEMBE KUWEKA MFUMO NA UONGOZI MPYA TAZARA.

WAZIRI wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na wafanyakazi wa Tazara, kulia ni naibu wake Dk. Charles Tizeba, na kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Tazara Damas Ndumbalo.




 Naibu Mkurugenzi wa Tazara Damas Ndumbalo akifafanua jambo kwa Waziri wa Uchukuzi.
Na MO BLOG
WAZIRI wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe ameapa kulinusuru Shirika la Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) kwa kufumua uongozi uliopo na kuweka uongozi mpya sanjari na kubadiliha mfumo wa uendeshaji shirika hilo.
“Matatizo yanayoikabili Tazara ni uongozi mbovu  hakuna cha Zambia wala Tanzania,hili tutalitafutia mwarubaini kwa hapa nchini lipo chini yangu na kwa Zambia ni la mamlaka nyingine,”alisema Mwakyembe.
Awali Katibu Mkuu wa (Trawu) Erasto Kiwele alitoa madai ya wafanya kazi ambapo alisema wanadai mishara ya miezi miwili na kumtaka Waziri Dk Mwakyembe kutumia uwezo wake kuwaondoa kwenye nyadhifa zao Mkurugenzi Mtendaji wa Tazara na Naibu wake.


No comments:

Post a Comment