Wednesday, June 13, 2012

ABIRIA WANUSURIKA KUFA BAADA YA KUTOKEA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MATATU LEO ASUBUHI.



Pichani Juu na Chini ni ajali hiyo ulivyokuwa.

Mmoja wa majeruhi akipewa msaada wa kupepewa na wasamaria wema baada ya kuzirai. Pichani Chini ni Askari wa Usalama Barabarani akichukua maelezo baada majeruhi huyo kuzinduka.


Askari wa kikosi cha uokoaji cha Ultimate Security wakitoa msaada.



Dereva wa Gari aina ya Alteza Zuhura Nyamatama (wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa askari wa usalama Barabarani jinsi ajali hiyo ilivyotokea.

Zuhura Nyamatama mkazi wa Kunduchi akifanya mawasiliano baada ya kunusurika kifo katika ajali iliyotokea leo asubuhi hii na kuhusisha gari tatu. Hata hivyo amelalamika kupata maumivu ya kifua

Abiria kadhaa wamenusurika kufa baada ya kutokea ajali iliyohusisha magari mawili ya abiria ‘daladala’ aina ‘coaster’ na gari dogo aina ya Toyota ALTEZZA.
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi majira ya saa 2:40 katika eneo la barabara ya Kaunda karibu njia panda ya kwenda Masaki.
Kwa mujibu wa Jofrey Mwakibete wa Mo Blog aliyekuwa mmoja wa abiria katika daladala hizo, daladala yenye nambari T 786 BWS iliyumba na kuigonga gari ndogo yenye nambari T 203 BXH iliyokuwa ikiendeshwa na Bi. Zuhura Nyamatama, na kisha kuigonga daladala nyingine iliyokuwa mbele yake.
Baada ya kusababisha ajali hiyo dereva na kondakta wa gari walikimbia.
Hata hivyo hakuna mtu aliyepoteza maisha ila abiria kadhaa wameruhiwa kutoka na ajili, wengine kutokana na kukanyagana waking’ang’ania kutoka nje huku wengine wakipata mshituko.
chanzo cha habari Na.MO BLOG TEAM



No comments:

Post a Comment