Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya shindano la Redds Miss World Tanzania 2012 litakalofanyika jijini Dar Es Saam katika ukumbi wa 324 Club uliopo Mikocheni jumamosi 16/06/2012,Kushoto ni Mkuu wa Itifaki wa Kamti ya Miss Tanzania, Oscar Makoye na Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International ambao ndio waandaaji wa mashindano ya urembo hapa nchini, Hashim Lundenga. Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji cha Redds ndio wadhamini wakuu wa Miss Tanzania.
********
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo imetangaza rasmi kudhamini shindano la kumpata mrembo atakewakilisha taifa katika mashindano ya urembo ya Dunia mwaka huu, yanayojulikana kama “Miss Wold 2012.
Akizungumzia Udhamini wa shindano hilo linalojulikana kama “Redd’s Miss World 2012” Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International ambao ndio waandaaji wa mashindano ya urembo hapa nchini Bw. Hashim Lundenga alisema; Ninajua wadau wengi wa tasnia ya urembo watastuka kuona mabadiliko haya, hii inatokana na kubadilika kwa ratiba ya mashindano ya Miss World toka mwezi wa December ilivyokuwa ikifanyika awali na sasa yatakuwa yakifanyika mwezi Julai hivyo kuwa na tofauti kubwa na ratiba ya mashindano yetu ya Redds Miss Tanzania ambayo huanza mwezi Mei na kumalizika Septemba.
Ili tusipoteze nafasi yetu ya kushiriki mwaka huu, kamati ya Miss Tanzania kwa ridhaa ya Serikali, iliamua kufanya shindano dogo “Mini competition” ambalo litatupatia mshindi atakae wakilisha Taifa katika mshindano hayo makubwa Duniani.
Warembo 10 wataingia kambini tarehe 13 hadi tarehe 17 June, na shindano litafanyika siku ya Juma Mosi tarehe 16 June katika ukumbi mpya wenye hadhi ya kimataifa wa 327 Club, uliopo Mikocheni.
Mshindi atazawadiwa pesa taslim shilingi Milioni mbili, na kupatiwa maandalizi yote kwa ajili ya matayarisho ya safari yake kwenda kwenye mashindano ya Miss World 2012 yatakayofanyika Inner Mongolia – China.
Kutokana na umuhimu wa kufanya shindano hili tuliwaomba wadhamini wakuu wa Miss Tanzania, kinywaji cha Redds ili watuwezeshe kufanikisha mchakato huu, nao bila kusita wakakubali. Hivyo tunawapongeza sana Redds kwa mchango wao mkubwa katika tasnia ya Urembo hapa nchini.
Akizungumzia maandalizi ya shindano hilo, meneja wa kinywaji cha Redds, Bi. Victoria Kimaro alisema; kwa upande wetu Redds, maandalizi yote yapo tayari, tunatarajia kuwa na shindano lenye mvuto wa aina yake, na litakuwa ndani ya ukumbi mpya wa kimataifa wa 327 kama mlivyosikia. Shindano hili litaanza saa Mbili usiku hadi saa Nne na litakuwa kwa waalikwa tu. Tumeandaa burudani za kutosha na tuna uhakika waalikwa watakaokuja kushuhudia mchakato huu wataridhika na maandalizi haya.
Mabadiliko haya ya ratiba za Miss World yataathiri ratiba zetu kwa mwaka huu tu, lakini yatakuwa na matunda mazuri kwetu kwa siku za usoni, kwani Redds Miss Tanzania atakaeshinda mwaka huu atapata muda mwingi na wa kutosha kujiandaa kwa ajili ya mchakato wa mashindano yajayo ya Miss World.
Tuna imani kubwa kuwa wadau wa tasnia ya Urembo wataonesha ushirikiano wao katika kufanikisha shindano hili na yote yajayo, ili kuinua tasnia ya Urembo hapa nchini.
No comments:
Post a Comment