Friday, June 22, 2012

BancABC YACHEZESHA DRAW YA WEKAWEKA UPATE

Kiongozi wa kitengo cha huduma za Benki kwa watu binafsi,biashara ndogona za kati wa BancABC, Ruth Makombe akimvalisha helmeti Naibu Mkurugenzi wa Benki  hiyo wakati wa kuchezesha droo ya bahati na sibu kwa wateja promosheni ya Wekaweka upatena BancABC iliyochezeshwa makao kwenye tawi la benki hiyo Upanga Dar es Salaam jana.Aliyekaa kwenye pikipiki ni Naibu Mkurugenzi Misheck Ugaro.
BancABC leo hii imehitimisha promosheni yake ya Wekaweka Upate na BancABC kwa kuwapata washindi kwa bahati nasibu iliyo chezeswa asubuhi hii. Bahati nasibu hiyo ilichezeshwa mbele ya wanahabari na wawakilishi wa Bodi ya Bahati nasibu ya Taifa katika tawi la BancABC lilipo Upanga, Dar Es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Bi. Ruth Makombe, ambaye ni kiongozi wa kitengo cha huduma za benki kwa watu binafsi, biashara ndogo na za kati alieleza kwamba promosheni ya Wekaweka Upate ilianza rasmi mwezi wa Novemba mwaka jana ambapo watu mbalimbali walipata nafasi ya kufungua akaunti katika matawi mbalimbali ya BancABC. Bi Ruth alisema, “Promosheni hii ilikuwa na lengo la kuwapatia wateja wetu nafasi ya kufikia ndoto zao kwa kuwapatia namna ya kutunza pesa zao huku wakijipatia mikopo, pia bila kusahau nafasi ya kujishindia zawadi nzuri zilizotolewa leo mbele yenu”. Promosheni ya Wekaweka ilikuwa na akaunti za aina mbili yaani Jipange Account na Fixed Deposit account ambapo zote mbili zilimuwezesha mteja kupata mkopo wa hadi kufikia asilimia 80 ya akiba yake kwa riba nafuu sana. Bi Ruth aliendelea kusema, “Kivutio kikubwa ni kwamba pamoja na kupata mkopo kwa akiba aliyoweka, mteja wetu pia anapokea riba ya kiasi cha fedha alichoweka kwenye account yake.”  “Leo hii tumehitimisha promosheni hii, lakini mpango wa wekaweka bado upo na unaendelea ili kuendeleza faida zake kwa wateja wetu”



Naye Bw. Mwalimu Zubery ambaye ni kiongozi wa kitengo cha fedha alisema anawashukuru wateja wote waliojiunga na promosheni hiyo kwa kufungua account na kuwaomba waendelee kufurahia huduma bora za BancABC. Aliendelea kusema kwamba, “Leo hii tuko hapa kwa ajili ya kutimiza ahadi yetu ya kuwazawadia washindi watatu ambao kila mmoja ataondoka na zawadi kabambe. Mshindi wa tatu atajipatia zawadi ya Generator, mshindi wa pili atajipatia Pikipiki na Mshindi wa kwanza atajipatia tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi katika nchi mojawapo ya mashariki ya kati/mbali (China, Singapore, Dubai, Uturuki na Thailand).


Bi Evelyn Auguste, Afisa Masoko wa BancABC alimalizia kwa kusema, “Tunapenda kuwashukuru wateja wetu wote kwa kuchagua BancABC, tunapenda kuwatangazia watanzania kutembelea matawi yetu yaliyopo hapa Dar Es Salaam na lile la mtaa wa Swahili mkoani Arusha ili kufurahia ubora wa huduma zetu, hasa hasa huduma yetu ya Kadi ya VISA ya malipo ya kabla ambapo mtu yeyote anaweza kupatiwa bila hata ya kuwa na account ya benki”.


No comments:

Post a Comment