Na.Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeendesha semina ya siku moja kwa majaji wa shindano la Epic Bongo Star Search 2012 kwa kuwataka kuzingatia maadili ya kazi zao.
Mratibu wa matukio wa Basata Malimi Mashili amewataka majaji hao kutambua kuwa asilimia kubwa ya washiriki wanategemea zaidi msaada wao katika kukuza vipaji.
Mashili aliwataka majaji hao kutambua kuwa mazingira waliyotoka washiriki na kuangalia namna ya kuwasaidia kulingana na mikoa yao kwa kuwa wapo ambao wana vipaji lakini wanatatizwa na suala la kuyazoea mazingira.
Amesema kwa kuwa mwaka huu EBSS itaruhusu washiriki wa miaka 16 hivyo ni vema zaidi wakazingatia suala la sauti kulingana na umri wa mshiriki sababu watakuwepo wenye sauti za kitoto pia.
Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 16 katika ukumbi wa Royal Village.
Majaji wa shindano hilo waliohudhuria ni pamoja na Jaji Mkuu Ritha Paulsen, Master Jay, Salama pamoja na mratibu wa EBSS kutoka Basata Vicky Temu.
No comments:
Post a Comment