Ofisa tawala katika ofisi ya mkaguzi wa mahesabu ya serikali Bi. Rosemary Michael (katikati) akitoa nasaha zake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katibu tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan kufungua mafunzo ya wiki tatu ya wakaguzi kutoka mikoa ya Singida,Morogoro,Dodoma,Tabora na Kigoma. Wa kwanza kulia ni katibu tawala mkoa wa Singida Liana Hassan na kushoto ni mwanasheria mkuu wa serikali mkoani Singida Rehema.
Katibu tawala mkoa wa Singida Liana Hassan akizungumza kwenye hafla ya kufungua mafunzo ya wiki tatu yanayohudhuriwa na wakaguzi wa mahesabu ya serikali.
Baadhi ya wakaguzi wa mahesabu ya serikali wanaohudhuria mafunzo ya wiki tatu yanayoendelea mjini Singida.
Katibu tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan (mwenye koti jeusi mstari wa mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wakaguzi wa mahesabu ya serikali wanaohudhuria mafunzo ya wiki tatu mjini Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na.Nathaniel Limu
Wakaguzi wa mahesabu ya shirika (NAO), wamehimizwa kuongeza kasi katika utekelezaji wa majukumu yao , kwa madai kwamba sasa imani na macho ya wananchi yako kwao.
Wito huo umetolewa na Katibu tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan, wakati akifungua mafunzo ya wiki tatu tanayohudhuriwa na wakaguzi 55 wa hesabu za serikali, kutoka mkoa wa Dodoma , Morogoro, Singida, Tabora na Kigoma.
Alisema hivi sasa ofisi ya ukaguzi wa mahesabu ya serikali, ni gumzo kila mahali kuanzia mijini hadi vijijini, kwa wasomi na wale wasiokuwa wasomi.
Liana alisema hali hiyo, ni ishara tosha kwamba sasa mnapaswa kutekeleza majukumu yenu kwa nguvu zaidi, ili imani ya jamiii iliyojengeka kwenu, iendelee kuimarika zaidi.
“Mafanikio haya yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na ofisi ya mkaguzi wa mahesabu ya serikali (NAO) kujikita zaidi katika kuhakikisha ina wafanyakazi wenye taaluma stahiki, na mara kwa mara, inawapa mafunzo mapya ili kukabiliana na mabadiliko ya mifumo mipya ya mahesabu ya serikali”,alisema.
Kwa upande wa wanamafunzo hao, Katibu tawala huyo aliwataka kutumia mafunzo hayo kujifunza zaidi na kubadilishana uzoefu lengo likiwa ni kuboresha utendaji wenu.
Awali afisa tawala wa ofisi ya mahesabu ya serikali makao makuu, Rosemary Michael, alisema mafunzo hayo ambayo yanafanyika pia sehemu mbali mbali nchini, lengo lake ni kuwajengea uwezo zaidi wakaguzi, ili waweze kutafisiri vizuri mifumo mbali mbali inayotumika kwenye mahesabu ya serikali.
“ Kama mnavyofahamu kwamba hivi sasa teknolojia inakuwa kwa haraka na inabadilika mara kwa mara. Kutokana na ukweli huo, wakaguzi wetu ni lazima tuhakikishe wanakwenda sambamba na mabadiliko hayo”alisema ofisa huyo.
No comments:
Post a Comment