Thursday, June 21, 2012

DROGBA ASAINI KLABU YA SHANGHAI SHENHUA, CHINA.

Aliyekuwa mshambulizi matata wa Chelsea Didier Drogba amehamia klabu ya Shanghai Shenhua ya China.
Kujiunga na klabu hicho , kimemfanya awe timu moja na mchezaji mwengine wa Chelsea Nicolas Anelka.
Mchezaji  huyo raia wa Ivory coast amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu na timu hiyo ya China.
Drogba mwenye umri wa miaka 34 amesema kabla ya kuamua kuhamia China alifikiria kwa makini sana.
“Nilitilia maanani mialiko mbalimbali niliopata katika kipindi cha wiki chache zilizopita , lakini nafikiri kwa wakati huu kuhamia timu ya Shanghai Shenhua ulikuwa uamuzi mzuri”


No comments:

Post a Comment