Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisoma Hotuba Bungeni Mjini, Dodoma Juni 25, 2012.
--
UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa Hoja kwamba kutokana na Taarifa zilizowasilishwa leo ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala na Kamati ya Fedha na Uchumi zilizochambua Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge lako sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2011/2012 na Mwelekeo wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2012/2013. Vilevile, naliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Taasisi zilizo chini yake pamoja na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2012/2013.
2. Mheshimiwa Spika, tangu tulipohaitimisha Mkutano wa Bajeti wa Bunge hili mwaka jana, Nchi yetu imekumbwa na Majanga na Matukio mbalimbali yaliyosababisha vifo na uharibifu wa mali. Nitumie fursa hii kutoa pole kwa wote waliofiwa na Ndugu, Jamaa na Marafiki. Mungu azilaze Roho za Marehemu mahali Pema Peponi. Kwa ndugu zetu walioumia na bado wanajiuguza, tumwombe Mwenyezi Mungu awasaidie kupona haraka na kurejea katika shughuli za ujenzi wa Taifa.Kusoma Hotuba hii ya Waziri Mkuu Bofya na Endelea Hapa......>>>>>>
No comments:
Post a Comment