Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam pamoja na mafanikio mengine limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa wizi kwenye mashine za ATM za benki mbali mbali.
Akitoa taarifa ya Jeshi hilo leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum – Dar es Salaam Kamanda Suleiman Kova amesema mtuhumiwa huyo Gode Pendacowsk mwenye umri wa miaka 28 raia wa Makidonia, amekamatwa kwenye hoteli ya Lamada akiwa na vifaa mbali mbali anavyofanyia uhalifu pamoja na laptop 5.
Katika hatua nyingine Kamada Kova amesema Jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata bunduki moja aina ya Short Gun Greener na risasi 5 na pia Bastola 5 pamoja Magari 18 jijini Dar es Salaam katika matukio tofauti.
Amesema katika tukio linguine polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wamefanikiwa kukamata mifuko 280 ya Mbolea ya Urea mali ya kampuni ya Nyombo Investment ya nchini Zambia inayokadiriwa kuwa na nathamani ya shilingi Milioni 48 za Tanzania.
Aidha kamanda Kova amesema Jeshi hilo pia limekamata noti za Tanzania na Dola za Marekani bandia zenye jumla ya thamani ya shilingi Milioni Thalathini na Tano na Laki Sita (35,600,000/-).
CHANZO NA MO BLOG TEAM
No comments:
Post a Comment