Thursday, June 14, 2012

KIPINDI CHA MASWALI NA MAJIBU WAKATI WABUNGE WAKISUBIRI KUSOMWA KWA BAJETI LEO.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisikiliza swali kutoka kwa  kiongozi wa Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe, Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu wa Mambo ya Ndani ya Nchi Pereira Ame Silima  akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na Wabunge katika kipindi cha maswali na majibu leo mjini Dodoma
Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu , Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI)  Aggrey Mwanri  akijibu maswali mbalimbali yaliulizwa na Wabunge katika kipindi cha maswali na majibu mjini Dodoma. 
Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA na Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe akimuuliza Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda maswali ya papo kwa papo leo mjini Dodoma katika kikao cha tatu cha mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano unaoendelea mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda (kulia) akimsikiliza kwa makini Waziri ujenzi Dkt. Jojn Pombe Magufuli(kushoto) leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao cha tatu cha mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoendelea mjini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa serikali  Jaji Fredrick Werema (kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi(kushoto) wakijadiliana jambo  leo mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu ) Stephen Wasira  akiwasilisha Bungeni  leo mjini Dodoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2011 na mwelekeo wa mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2012/13.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Sengerema Mh. William Ngeleja kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wanachuo wa Chuo cha Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa cha Hombolo, Dodoma kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Emmanuel Nchimbi (katikati) , Mbunge wa Afrika Mashariki Shyrose Bhanji (kulia) na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Esther Bulaya(kushoto) wakibadishana mawazo leo mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu na  Tiganya Vincent-MAELEZO- Dodoma).

No comments:

Post a Comment