Thursday, June 14, 2012

VURUGU ZILIZOTOKEA POLAND NI ZAO LA HISTORIA BAINA YAO NA WARUSI.


Zaidi ya mashabiki kumi wa mpira wamejeruhiwa na wengine 140 kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kusababisha vurugu katika mji wa ‘Warsaw’ wakati wa mechi ya Russia na Poland .
Televisioni zilionesha mashabiki wakihaha na kukimbia ovyo milipuko ya moto katika mitaa. Wakati wengine wakionekana kutokwa damu sababu ya majeraha.
Mchezo huo ulipangwa siku ya Uhuru wa Russia na kabla haujaanza bendera kubwa iloshikwa na mashabiki ilionekana na maneno yaliyomaanisha “Hi indio Urusi”
Historia ya nchi hizi mbili ni ngumu kwasababu ya utawala wa Urusi dhidi ya Poland wakati wa vita baridi ‘Cold War’
Polisi wamesema bado wanaangalia kupitia CCTV watu zaidi waliohusika na tukio hilo, ambalo ni baya zaidi katika historia ya mashindano hayo makubwa Ulaya “UEFA, EURO 2012”.
CHANZO MO-BLOG


No comments:

Post a Comment