Friday, June 22, 2012

KUTOKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA LEO.


Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dkt. Makongoro Mahanga(kushoto) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige  wakati wa mapumziko ya mchana ya Bunge la Bajeti  linaloendelea mjini Dodoma. 
Baadhi ya wabunge wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakijaza fomu za vitambulisho vya Taifa leo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda(katikati) akibadilishana mawazo jana  na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (kushoto) MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (kulia),wakati wa mapumziko ya mchana ya kikao cha Bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma.
Wakufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi ngazi ya kitaifa wakishiriki katika mafunzo ya  kujaza dodoso fupi la sense ya watu na makazi leo katika mafunzo ya siku 10 yanayoendelea mjini Dodoma. Mafunzo hayo yameandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakufunzi hao ili nao waweze kuendesha katika ngazi za mikoa mbalimbali hapa nchini.(Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO-Dodoma).


Mbunge wa Mbeya Mjini joseph Mbilinyi (SUGU) akibadilishana mawazo na Mbunge Mwenzie kutoka Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe leo wakati wa mapumziko ya mchana ya Bunge la Bajeti  linaloendelea mjini Dodoma.



No comments:

Post a Comment