Na. Luppy Kung’alo, Dodoma
Jeshi la Polisi Mkoani DodomaJeshi la Polisi Mkoani Dodoma limemkamata mtu mmoja, aliyefahamika kwa jina la MWANGA S/O MSEMAKWELI mwenye umri wa miaka 41, Mkulima, Mkazi wa Ising’ht kwa tuhuma za kulima Bhangi katika shamba lake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen alisema tukio hilo lililotokea tarehe 14/06/2012 majira ya saa 09:00 asubuhi katika kijiji cha Insig’ht Wilaya ya Mpwapwa Mkoni Dodoma, baada ya Jeshi la Polisi kupitia Mkakati wa Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kupokea taarifa toka kwa wanakijiji wema kuwa kuna mtu analima bangi katika shamba lake.
“Mkulima huyo wa bangi alikuwa amelima mazao ya Mahindi na Alizeti pembezoni kulizunguka shamba lake na katikati alilima bangi ili kufanya wanakijiji wenzake wasimgundue kuwa analima bangi.” Alisisitiza Kamanda Zelothe
Bw. Zelothe Stephen alisema iliwashangaza wanakijiji na wakulima wenzake kuona wao wamevuna mazao yao katika mashamba yao lakini mwenzao alikuwa hajavuna, hivyo kumtilia shaka na kumfuatilia na hatimaye kutoa taarifa Polisi ambao walikwenda kumkamata.
Mkuu huyo wa Polisi Mkoa wa Dodoma alisema baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa hizo, walijipanga na kwenda kumkamata mtuhumiwa na kisha kumpekua nyumbani kwake na kumkuta na kete kumi na tisa za bangi pamoja na bangi iliyokuwa haijasokotwa ikiwa kwenye mfuko wa Nailon ambapo ilipopimwa ilikutwa ni gram mia tano.
Aidha Bw. Zelothe alisema Jeshi la Polisi Wilayani Mpwawa kwa kushirikiana na wanakijiji cha insig’ht Walifanikiwa kuliteketeza kwa moto shamba hilo la bangi lenye ukubwa wa hekali mbili.
Kamanda Zelothe Stephen alitoa wito kwa wakulima kuacha kulima zao hilo la bangi kwani ni kinyume na sheria za nchi na kuahidi kwamba mkulima yeyote atakayegundulika kulima zao hilo, hatua kali na za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Wakati huo huo Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma alisema mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Allen s/o Kibwana mwenye umri wa miaka (44) Mgogo, mkulima mkazi wa kitongoji cha mbande madukani, kata ya sajeli tarafa ya kongwa na wilaya ya kongwa amekutwa amejinyonga nyumbani kwake.
Kamanda Zelothe Stephen alisema tukio hili litokea jana tarehe 15/06/2012 majira ya 06:00 asubuhi, ambapo mtu huyo alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani.
Bw. Zelothe Stephen alisema marehemu ameacha ujumbe wa barua ukieleza kuwa sababu ya kujinyonga kwake kuwa ni mizozo ya muda mrefu na mkewe na ndugu zake akiwatuhumu kupanga njama za kummaliza ki mapato.
No comments:
Post a Comment