Wednesday, June 20, 2012

VODACOM YATOA POLE KUFUATIA KIFO CHA MHARIRI WA JAMBO LEO.


-Yasema ni pigo kubwa kwa wadau wa habari
-Yawataka wanahabari kumuenzi
Kampuni ya simu ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha ghafla cha mwanahabari mahiri Bw. Willy Ogunde Edward kilichotokea usiku wa kuamkia Jumatatu wiki hii.
“Tunatoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu, waajiri wake na kipekee familia ya wanahabari nchini kwa kuondokewa na mpiganaji na kamanda wetu aliyekuwa sehemu muhimu ya ujenzi wa tasnia ya habari nchini.”Alisema Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza
Marehemu Willy Edward alikuwa ni mdau wa habari mwenye msaada na ushauri pale anapohitajika na aliiwakilisha vyema tasnia hii ya habari tangu alipokuwa Majira mpaka kabla umauti haujamkuta akiwa Mhariri wa habari wa Jambo Leo.
Marehemuatakumbukwa kwa jinsi ambavyo alikua mahiri katika kazi yake, ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na kwamba mchango wake utaendelea kuwa chachu hasa kwa vizazi vijavyo vya wanahabari chipukizi nchini.
“Tutamkumbuka sana Marehemu Willy ambae alikuwa ni mpole na mcheshi na mwenye utashi wa mafanikio katika kazi zake. Hakusita kutoa ushauri kuboresha uandishi wa habari ili kutoa ujumbe uliokamilika na sahihi pale alipoona mapungufu kutika habari husika”. Alisema Meza.
Mkurugenzi huyo Mkuu wa Vodacom amesema kampuni yake daima ina thamini na kuheshimu mchango wa wanahabari katika maendeleo ya taifa na uimarishaji ustawi wa jamii na kuamini kuwa wanahabari waliobaki wataendeleza urithi (Legacy) aliouacha marehemu Willy.
Mungu azilaze roho za Marehemu BwWilly Ogunde Edward mahali pema peponi –Amen

No comments:

Post a Comment