Wednesday, June 20, 2012

MAELEZO YA BAJETI KIVULI-ZITTO KABWE.

Zitto akiwasili Bungeni kwa ajili ya kwenda kuwasilisha bajeti ya upinzani.

Zitto akiwasilisha hotuba ya bajeti kivuli.
Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.
 MAPATO
SHILINGI MILIONI
AMapato ya ndani
 
11,889,078
 i)mapato ya kodi (TRA)
10,232,539
 ii)Mapato yasiyo ya kodi
1,163,533
BMapato ya Halmashauri
493,006
Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu.
Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.
Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.
Kabwe Zuberi Zitto,Mb
Waziri wa Fedha na Uchumi Kivuli
19.06.2012


No comments:

Post a Comment