Wednesday, June 6, 2012

WABUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI WALA KIAPO.

Mh. Samuel Sitta ni muwakilishi wa Tanzania.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Shy-Rose Banji akila kiapo chake.

Mh. Alhaji. Adam Kimbisa.
Mhe. Anjela Charles Kizigha.
Mhe. Bernard Musomi Murunyana.
Mh. Abdullah Ali Hassan Mwinyi.


Mh.Charles Makongoro Nyerere.

Mh. Dkt. Twaha Issa Taslima.
Mh.Nderkindo Perpetua Kessy. SOURCE: FATHER KIDEVU BLOG
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) jana wameapishwa rasmi kushika madaraka hayo huku Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hulo.
Wabunge hao waliapa baada ya kupatikana Spika wa mpya wa Bunge hilo ambapo safari hii ikiwa ni Uganda kushika Uongozi huo wa Juu wa Bunge na Mwana Uchumi, Margareth Zziwa kuchukua nafasi hiyo.
Wabunge wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki waliokula kiapo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge EALA, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh. Shy-Rose SaddrudinBhanji.
Wengine ni Mhe. Anjela Charless Kizigha, Mh. Maryam Ussi Yahya, Mh.Nderkindo Perpetua Kessy,  Mh.Dkt.Twaha Issa Taslima, Mhe. Abdallah Ali Hassan Mwinyi, Mhe Bernard Musomi Murunyana Mhe. Charles Makongoro Nyerere na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta anaeingia kwa wadhifa wake wa Uwaziri.
Wabunge hao wameapisha pamoja na wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.


No comments:

Post a Comment