Friday, June 22, 2012

WAREMBO MISS DAR INTERCOLLEGE WAFUNDWA.

Kamati ya Miss TAnzania imetembelea kambi ya Miss Dar Intercollege iliyopo kwenye hoteli ya The Grand Villa, Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwafunda.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika ijumaa ya kesho katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala na chuo cha Usmiamizi wa Fedha (IFM).
Akizungumza na warembo hao, mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye aliwataka warembo hao kufuata miongozi na kanuni za shindano hilo ikiwemo kuwa na nidhamu.
Alisema urembo si sura na umbo zuri bali unahusisha pia nidhamu katika jamii hivyo amewataka warembo hao kuzingatia hayo.
“Nafahamu ninyi ni wasomi wazuri hivyo mmeyapokea vema mafunzo tuliyowapa…hatutarajii kusikia mmoja wenu anachafua hali ya hewa katika siku za usoni na mambo ya skendo skendo,”Alisema Makoye.
Dina alisema shindano hilo litapambwa na msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasib Addul ‘Diamond’ sambamba na bendi ya Skylight iliyopo chini ya mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba.
 “Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.
Warembo watakaoshiriki shindano hilo  wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time,  Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM)  na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.
Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel,Grand Villa Hotel, Sporti Kizaa zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi, dina ismail (zamani Mamapipiro), Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe


No comments:

Post a Comment