Warembo waliojitokeza kuwania nafasi ya Kuiwakilisha Tanzania katika shindano la mwaka huu la Miss World 2012, wanaendelea na mazoezi yao katika kambi yao iliyopo Hoteli ya Giraffe Ocean View nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Shindano hilo maalum lijulikanano kama Redds Miss World Tanzania 2012 linataraji kufanyika siku ya Jumamosi June, 2012 katika ukumbi mpya wenye hadhi ya kimataifa wa 327 Club, uliopo Mikocheni.
Warembo waliongia kambini na Kunolewa na Miss Tanzania 2011, Salha Izrael ni pamoja na
1. Gloryblaca Mayowa (Lindi)
2. Hamisa Hassan (Kinondoni)
3. Queen Saleh (Ilala)
4. Christine Willium (Iringa)
5. Pendo Laizer (Arusha)
6. Lisa Jensen (Mara)
7. Mwajabu Juma (Temeke)
8. Neema Saleh (Ilala)
9. Jeneffer Kalolaki (Ilala)
10. Stella Mbuge (Kinondoni)
Mshindi atazawadiwa pesa taslim shilingi Milioni mbili, na kupatiwa maandalizi yote kwa ajili ya matayarisho ya safari yake kwenda kwenye mashindano ya Miss World 2012 yatakayofanyika Inner Mongolia – China.
washiriki hao wakiwa katika picha ya pamoja na mwalimu wao Miss Tanzania 2012, Salha Izrael.
PICHA HABARI NA FATHER KIDEVU
No comments:
Post a Comment