Bia ya Ndovu Special Malt inayotengenezwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), leo imezindua muonekano wake mpya ambao umeiongezea bia hiyo yenye hadhi ya juu hapa nchini na kimataifa mvuto zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo uliofanyika Jijini Dar es Salaam, meneja wa Bia ya Ndovu Bi. Pamela Kikuli alisema; Tunayo furaha kubwa sana siku ya leo kuzindua muonekano mpya wa Bia hii ya Ndovu Special Malt.
Lengo kuu la maboresho haya yaliyofanyika ni kuipa Bia hii ya Ndovu muonekano wenye mvuto zaidi, lakini pia kuvipa muonekano zaidi vitu muhimu vinavyoitambulisha bia hii.
Ukiangalia katika lebo ya mbele, picha ya mnyama Tembo, au kwa jina jingine Ndovu imeongezwa ukubwa, hii ni kwa sababu maalum za kumpa uzito unaostahili mnyama huyu ambae ndio kitambulisho namba moja cha bia hii. Maboresho mengine yaliyofanywa ni pamoja na kuboresha nembo ya kiungo muhimu kinachoitofautisha bia ya Ndovu na bia nyingine “Cristal Malt”, pia lebo inayozunguka shingo ya bia hii (foil) ambayo sasa ina mg’ao angavu wa dhahabu. Wapenzi wa Bia hii ya Ndovu special Malt watapata pia historia ya bia hii katika lebo ya nyuma hivyo kuwawezesha kuielewa bia yao vizuri zaidi. Tunatarajia maboresho haya yatawavutia zaidi wadau wa Ndovu Special Malt na hivyo kuongeza mafanikio ya bia hii. Alisema Pamela.
No comments:
Post a Comment