Monday, May 21, 2012

AJISHINDIA PIKIPIKI KUPITIA BAHATI NASIBU YA YANGA

Meneja wa Kampeni ya Bahati Nasibu ya SMS ya Yanga, Talib Rashid (katikati) akichezesha bahati nasibu hiyo jana makao makuu ya klabu hiyo ambapo Rhobi Revocatus wa Mwanza alishinda pikipiki. Kulia ni Afisa Habari wa Yanga, lousi sendeu na kushoto ni Msimamizi wa bahati nasibu hiyo.
 *********
KAMPUNI ya Push Mobile kwa kushirikiana na klabu ya Yanga jana ilimpata mshindi wa bahati nasibu kwa mashabiki wa timu hiyo ambapo amejinyakulia zawadi ya Pikipiki yenye thamani ya sh mil 1.8.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana  Meneja wa Push Mobile Talib Rashid alisema kampeini hiyo ni ya siku 90 ambapo wamewapata washindi wengine 45 ambao watajinyakulia kitita cha sh 50,000.
Rashid alimtaja mshindi wa pikipiki kuwa ni mwana dada Robby Revocatius miaka(39) mkazi wa Mwanza Kilimahewa na kumpigia simu hapo hapo kumjulisha kuwa yeye ndiye aliyeibuka mshindi katika kampein hizo.
“Mshindi tumemtafuta hapa hapa na nyie mmeshuhudia na ninampigia simu mbele yenu ili aweze kuzungumza kwa namna ambavyo amepokea ushindi huo”alisema Rashidi na kuongeza kuwa siku 40 zijazo mshindi atajinyakulia bajaji.
Mra baada ya Rashid kupiga simu namba 0789220556 alipokea muhusika na kusema kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Yanga na kusema kuwa hata juzi katika mkutano wa wazee na wanachama alitamini angefika.
“Mimi siamini kama nimeshinda na mimi ni shabiki mkubwa wa Yanga na hata tulivyofugwa mabao 5 na mtani wetu niliumia sana ila kaka pikipiki hata sijui kuendesha itakuwaje”alisema Robby mara baada ya kupigiwa simu na kuambiwa kuwa ni mshindi.
Rashid alisema kuwa mshindi huyo atakabidhiwa pikipiki hiyo ndani ya wiki moja ijayo na kuwaomba wapenzi wa Yanga kujitokeza kwa wingi kushiriki ili na wao kuibuka washindi na kusema kuwa kujiunga unaandika neno Yanga kwenda namba 15678.
Kwa upande wa Yanga Ofisa habari ya klabu hiyo Louis Sendeu alisema kuwa wao kama Yanga wataendelea kutoa taharifa kwa Push Mobile na kuwataka wanaYanga kujiunga kwa wingi ili wapate mambo mengi ambayo yanaendelea kwa sasa katika kalbu hiyo.


No comments:

Post a Comment