Monday, May 21, 2012

FLAVIANA MATATA ATOA MSAADA WA MABOYA 500 KWA SHIRIKA LA MELI LA TAIFA JIJINI MWANZA


Historia imewekwa leo na Flaviana Matata alipokabidhi msaada wa maboya (life vests) 500 kwa Shirika la Meli la Taifa (Marine Services Co Ltd) kama sehemu ya kumbukumbu ya MV Bukoba - ambapo ni miaka 16 tokea meli hiyo ilizama na kuua watu takriban 1,000 akiwa pamoja na mama yake  
Baada ya makabidhiano, wakati wa hotuba, Flaviana Matata alishindwa kuendelea na hotuba yake baada ya kuzidiwa na majonzi ya kumkumbuka mama yake mzazi aliyempoteza katika ajali ya MV Bukoba miaka 16 iliyopita ...
Flaviana Matata akiweka shada kwenye kaburi isiyo na jina Igoma jijini Mwanza kama sehemu ya kumbukumbu ya watu waliopoteza maisha yao katika ajali ya MV Bukoba. Flaviana alimpoteza mama yake mzazi

habari kwa hisani ya blog http://mashughuli.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment