Aliyekuwa Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Raphael Koimere (mwenye suti), akizungumza baada ya kurejesha kadi ya chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willbrod Slaa (mwenye kofia), wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam leo. (Picha zote ma Joseph Senga).
Sehemu ya umati wa maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao walihudhuria mkutano wa hadhara wa chama hicho.
Baadhi ya viongozi wakuu wa Chadema, wakiwa katika jukwaa kuu kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara Jwangwani, Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche, Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje.
Magari yaliyowabeba viongozi wakuu wa Chadema yakilakiwa na baadhi ya wananchi wa jiji la Dar es Salaam, walipowasili kwenye Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam Jana.
Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje na mwanachama mpya wa Chadema, James Ole Millya wakilakiwa mara baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Jangwani.
Baadhi ya mabango ya yenye ujumbe mbali mbali pia yalikuwa ni sehemu ya vionjo vilivyojirika katika mkutano huo, kama yanavyoonekana pichani.
No comments:
Post a Comment