Sunday, May 27, 2012

WAMA YAWEZESHA WANAWAKE KUWAPA SEMINA KUHUSIANA NA UMUHIMU WA BIMA YA AFYA.

Tabu Likoko Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Wanawake katika Taasisi ya (WAMA) akifungua rasmi semina ya wanawake kutoka vikundi mbalimbali vya kuweka na kukopa vinavyosimamiwa na Taasisi ya (WAMA) kuhusu huduma za Mfuko wa Bima wa Afya NHIF inayofanyika kwenye viwanja vya Taasisi ya WAMA asubuhi hii jijini Dar es salaam kutoka kulia  pichani ni Rehani Athumani Mkurugenzi mifuko ya Afya ya Jamii (CHF), Michael Mhando Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai wa Mfuko na Utafiti na Eugen Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji.

Afisa wa Masoko na Elimu kwa Umma NHIF Grace Michael akifuatilia mada katika semina hiyo, kushoto ni Philomena Marijani Afisa Uraghibishi na Mawasiliano Taasisi ya (WAMA).

Eugen Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF) akizungumza katika semina hiyo jinsi mfuko huo unavyosaidia jamii kupata matibabu, kulia ni Rehani Athumani Mkurugenzi mifuko ya Afya ya Jamii (CHF) na katikati ni Michael Mhando Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai wa Mfuko na Utafiti.

Rehani Athumani Mkurugenzi mifuko ya Afya ya Jamii (CHF) akitoa mada mbalimbali juu ya huduma za mfuko wa bima ya Afya, huku washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza kwa makini, katikati ni  Michael Mhando Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai wa Mfuko na Utafiti na kulia Eugen Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji.



Tabu Likoko Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Wanawake katika Taasisi ya (WAMA) kulia na Philomena Marijani Afisa Uraghibishi na Mawasiliano Taasisi ya (WAMA) ambao ndiyo wenyeji wa wanasemina wakiwa katika semina hiyo.

No comments:

Post a Comment