Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa ufafanuzi kwa wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya kitaifa jana mjini Dodoma. Wakufunzi hao wanaandaliwa kwa ajili ya kwenda katika mikoa mbalimbali nchini kwa ajili ya kuwaelimisha wengi watakaosaidia kufanikisha zoezi la sensa tarehe 26 mwezi Agosti mwaka huu.
Kamishna wa Sensa Hajjat Amina Mrisho akitoa neno la utangulizi kwa wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya Kitaifa wakati wa mafunzo ya siku 10 tayari kwa ajili ya kwenda kufundisha hatua za mikoa . Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) yalianza jana mjini Dodoma.
Baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu na wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya Kitaifa wakiwa wametulia kimya kwa dakika mbili kwa ajili ya kuombeleza kifo cha Mhariri wa Jamboleo Willy Edward kilichotokea mjini Morogoro alipokuwa akihudhuria mafunzo ya sense kwa wahariri . Viongozi na wakufunzi hao walikuwa katika mafunzo ya siku 10 tayari kwa ajili ya kwenda kufundisha hatua za mikoa . Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)yalianza jana mjini Dodoma.
Baadhi ya wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya Kitaifa wakiwa katika mafunzo ya siku 10 tayari kwa ajili ya kwenda kufundisha hatua za mikoa wakifuatilia mafunzo kutoka kwa wataalam mbalimbali walikuwa wakitoa mada mbalimbali. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) yalianza jana mjini Dodoma.(Picha na Tiganya Vincent- Dodoma).
No comments:
Post a Comment